BAGHDAD: Watu na magari yapigwa marufuku barabarani | Habari za Ulimwengu | DW | 05.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Watu na magari yapigwa marufuku barabarani

Mji mkuu wa Irak,Baghdad umewekwa chini ya ulinzi mkali,huku mahakama maalum ikitarajiwa kumhukumu rais wa zamani Saddam Hussein.Saddam ameshtakiwa uhalifu dhidi ya binadamu kuhusika na mauaji ya takriban Washia 150 katika mwaka 1982.Wakuu wa Irak wana hofu kuwa wafuasi wa kiongozi huyo aliepinduliwa watafanya machafuko ikiwa atapewa adhabu ya kifo.Televisheni ya taifa imesema, kuanzia mapema Jumapili watu na magari ya yamekatazwa kutembea barabarani na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Baghdad unafungwa.Siku ya Jumamosi hadi watu 30 waliuawa katika mashambulio yaliofanywa na wanamgambo sehemu mbali mbali nchini Irak.Wakati huo huo wizara ya mambo ya ndani imesema,imewaua wanamgambo 35 nje ya mji mkuu Baghdad.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com