BAGHDAD : Watu 130 wauwauwa na zaidi ya 300 wajeruhiwa | Habari za Ulimwengu | DW | 04.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : Watu 130 wauwauwa na zaidi ya 300 wajeruhiwa

Takriban watu 130 wameuwawa na wengine zaidi ya 340 kujeruhiwa katika shambulio la kujitolea muhanga maisha mjini Baghdad.

Polisi imesema mshambuliaji aliendesha gari kubwa la mizigo lililosheheni tani moja ya mabomu na kujiripuwa kwenye soko lililojaa watu katika eneo linalokaliwa na Washia wengi mjini Baghdad.

Shambulio hilo ambalo Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al Maliki anawalaumu wafuasi wa Saddam Hussein na wanamgambo wa Kisunni limeteketeza vibanda vya matunda na mboga mboga na kupelekea miili ya watu kutapakaa njiani.

Shambulio hilo pia linakuja wakati wanajeshi wa Marekani na wa Iraq wakijiandaa kufanya shambulio la pamoja ikiwa kama ni juhudi za mwisho za kukomesha umwagaji damu wa kimadhehebu ambao umekuwa ukiuuwa mamia ya watu mjini Baghdad kila wiki.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com