1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Vikosi vimepambana na wanamgambo wa Kishia

8 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4n

Waasi 30 wameuawa na vikosi vya Kiiraki na Marekani katika mji wa Diwaniya wenye wakazi wengi wa Kishia.Taarifa iliyotolewa na jeshi la Kimarekani imesema mapigano yalizuka,wanajeshi wa Kiiraki na Kimarekani walipojaribu kumkamata mtu alielezwa kuwa ni muhimu sana.Taarifa hiyo imeongezea kuwa mshukiwa huyo amekamatwa,lakini jina lake halikutajwa.Eneo la kusini la Diwaniya ni ngóme ya wanamgambo wa “Jeshi la Mehdi” la kiongozi wa kidini wa Kishia,Moqtada al-Sadr. Amri ya kuwazuia watu kutoka nje imetangazwa katika mji huo.