BAGHDAD: Taarifa ya Marekani yasema hali ya Iraq inakatisha tamaa. | Habari za Ulimwengu | DW | 03.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Taarifa ya Marekani yasema hali ya Iraq inakatisha tamaa.

Taarifa ya hivi karibuni ya Marekani kuhusu hali ya usalama nchini Iraq inadhihirisha hali ya kukatisha tamaa nchini humo ikitahadharisha yamkini mambo yakazidi kuzorota iwapo juhudi za ziada hazitafanywa kukabiliana na ghasia.

Taarifa hiyo ya kijasusi inasema ghasia kati ya wafuasi wa madhehebu ya Sunni na Shia, zinazidi tishio la kundi la al-Qaeda, na kwa namna fulani ghasia hizo ni sawa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Serikali ya Rais George W. Bush imekuwa ikichelea kutumia kama hiyo kuelezea uhasama huo unaoendelea nchini Iraq.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com