1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD :Sherehe za Shabaniya zaanza Karbala

26 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVq

Maelfu ya mahujaji wa Kishia wamewasili mjini Karbala hii leo ili kuadhimisha kuzaliwa kwa Imam mmoja aliyepotea katika karne ya 9.Zaidi ya waumini milioni moja wa Kishia kutoka kote ulimwenguni wanatarajiwa kukutana kwenye mji huo tukufu kwa sherehe hizo zinazofikia kilelekesho kutwa jioni na asubuhi Jumatano.

Tamasha la Shabaniya zinaadhimisha kuzaliwa kwa Mohamed al Mahdi,Imam wa 12 wa Kishia na wa mwisho aliyetoweka katika karne ya 9.Kulingana na imani ya Kishia Imam huyo alinusurika kifo na atarejea Ulimwenguni ili kusambaza amani na sheria.

Wanaume 6 walijeruhiwa walipokuwa wakielekea mjini Karbala kwa miguu pamoja na mwanamke mmoja aliyepigwa risasi mjini Baghdad.Uongozi nchini Iraq umepiga marufuku matumzi ya baiskele,pikipiki na mikokoteni ya farasi katika barabara mjini Baghdad ili kuzuia ghasia ambazo huenda zikasababishwa na Wasunni walio na msimamo mkali.

Kwa mujibu wa msemaji wa mkuu wa jeshi mjini Baghdad Brigadia Jenerali Qassim al-Mousawial-Mousawi,majeshi ya Marekani na mengine ya kimataifa yatatoa huduma za maji safi kwa mahujaji hao walio safarini kuelekea Karbala.