1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mwanajeshi wa Kimarekani amekiri makosa ya kubaka na kuua

16 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsN

Mwanajeshi wa Kimarekani amekiri makosa ya kumbaka msichana wa Kiiraki na kuwaua watu watatu wa familia ya msichana huyo.Mwanajeshi huyo alikiri makosa hayo baada ya wakili wake wa utetezi kupata maafikiano ya kuzuia adhabu ya kifo na badala yake mwanajeshi huyo atoe ushahidi dhidi ya washtakiwa wengine watatu.Mauaji hayo yaliotokea Mahmoudiya,kijiji kilicho kama kilomita 30 kusini mwa Baghdad,ni moja kati ya mkururuo wa mauaji na matumizi mabaya ya nguvu yaliofanywa na majeshi nchini Irak dhidi ya raia.