BAGHDAD : Miripuko yaendelea kugharimu maisha | Habari za Ulimwengu | DW | 08.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : Miripuko yaendelea kugharimu maisha

Wimbi la mashambulizi ya mabomu laendelea kugharimu maisha nchini Iraq.

Mshambuliaji wa kujitolea muhanga maisha amejiripuwa kwenye lori na kuuwa makuruta 23 wa jeshi la Iraq na kujeruhi wengine 27 leo hii baada ya kulibamiza lori hilo na gari lao. Makuruta hao walikuwa ni wa madhehebu ya Sunni na ndio kwanza walikuwa wamejiunga na jeshi hilo la Iraq katika jimbo la magharibi la Anbar.

Mapema mashambulizi mawili ya mabomu yaliotegewa kwenye magari yameuwa watu wanane katika eneo la Karrada mjini Baghdad linalokaliwa na mchanganyiko wa Wasunni na Washia.

Wakati huo huo idadi ya vifo kutokana na mashambulizi matatu ya hivi karibuni ya kujitolea muhanga maisha kwa kujiripuwa kaskazini mwa Iraq imeongezeka na kufikia watu 150 na wengine 200 kujeruhiwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com