Baghdad. Mateka kadha watafuta na jeshi la Marekani. | Habari za Ulimwengu | DW | 19.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baghdad. Mateka kadha watafuta na jeshi la Marekani.

Majeshi ya Marekani na yale yanayoongozwa na Marekani yanawatafuta mateka kadha kusini mwa Iraq, baada ya Mmarekani mmoja aliyetekwa nyara kukutwa ameuwawa na wengine wawili kuokolewa katika msako siku ya Ijumaa.

Idadi kadha ya watu wa mataifa ya nje wamekamatwa hivi karibuni na wanamgambo waliovalia sare za polisi.

Polisi katika mji wa Baquba, kaskazini mwa Baghdad, wameweka marufuku ya kutotembea ovyo baada ya kutokea mashambulizi kadha .

Maafisa wa wizara ya mambo ya ndani wamesema kuwa makombora mawili yaliwauwa watu wawili na kuwajeruhi wengine watano.

Wakaazi wamesema kuwa mashambulizi hayo yalifuatiwa na mapigano makali baina ya wapiganaji na wanajeshi katika mitaa ya mji huo. Kumekuwa na ripoti za kutatanisha kuhusu idadi ya watu waliokufa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com