1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Marekani kubadili mbinu za usalama.

20 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0v

Jeshi la Marekani limetangaza kuwa litaangalia upya mkakati wake wa usalama kwa ajili ya mji mkuu wa Iraq Baghdad.

Taarifa hiyo inakuja wakati kumekuwa na idadi kubwa ya mashambulizi yanayofanywa na wapiganaji. Mabomu ya kujitoa mhanga katika magari, makombora na risasi za hapa na pale katika miji ya Mosul, Kirkuk na Khalis vimeuwa kiasi cha raia 38 pamoja na wanajeshi na kuwajeruhi kiasi cha watu 140 wengine jana Alhamis.

Akizungumza na waandishi wa habari waziri wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld amesema.

Maafisa wa wizara ya ulinzi pia wametangaza vifo vya wanajeshi wengine watatu wa Marekani, na kufikisha idadi ya wanajeshi 74 katika mwezi huu wa Oktoba.

Mwezi huu unakuwa mwezi mbaya kabisa kwa majeshi ya Marekani katika muda wa karibu miaka miwili.