BAGHDAD: Gavana na mkuu wa polisi wazikwa | Habari za Ulimwengu | DW | 12.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Gavana na mkuu wa polisi wazikwa

Wanajeshi wanne wa Marekani wameuwawa kwenye mlipuko wakati wa operesheni za kijeshi katika eneo la kusini mwa mji wa Baghdad.

Taarifa ya jeshi la Marekani imesema kwamba wanajeshi wengine wanne wamejeruhiwa kwenye mlipuko huo.

Hakuna taarifa zaidi zilizotolewa juu ya mlipuko huo.

Wanajeshi wengi wa Marekani wamepelekwa katika eneo la kusini mwa Baghdad kukabiliana na ongezeko la uingiaji wa silaha, milipuko na wapiganaji wenye msimamo mkali wa madhehebu ya Kashia na Kisunni wenye asili ya kiarabu kuelekea mji mkuu wa Baghdad.

Wakati huo huo mamia ya waombolezaji walihudhuria mazishi ya gavana na mkuu wa polisi wa mkoa wa Qadisiyah waliouwawa.

Waziri mkuu wa Irak Nuri al Maliki ametoa agizo la kuanzishwa uchunguzi wa mauaji hayo.

Polisi waliweka ulinzi mkali mahala palipofanyika maziko katika mji mtakatifu wa jamii ya Washia wa Najaf.

Mjini Baghdad katika ofisi ya waziri mkuu Nuri al Maliki kumefanyika dua ya maombolezo kwa ajili ya gavana Khalil Hamza na mkuu wa polisi Khalid Hassan waliouwawa katika shambulio la bomu. Walinzi wao watatu pia waliuwawa kwenye shambulio hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com