Bafanabafana yachapwa na Uruguay
17 Juni 2010Matangazo
Alikuwa ni mshambuliaji wa Uruguay Diego Folan aliyepachika mabao mawili kabla ya Avaro Pereira kupachika la tatu na kuiweka Bafanabafana nchani mwa fainali hizo.
Bafanabafana ilishuhudia mlinda mlango wake Itumeleng Khune akipewa kadi nyekundu.Kipigo hicho kilizima kelele za vuvuzela na kutoa nafasi kwa washabiki wa Uruguay kuimba.
Mapema Uswis iliushangaza ulimwengu wa soka kwa kuwafunga mabingwa wa Ulaya Uhispania bao 1-0.Uhispani ni miongoni mwa timu ambazo zinapigiwa upatu kutwaa kombe hilo.
Mwandishi:Aboubakary Liongo