1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ASUNCION: Rais wa Ujerumani ziarani Paraguay

6 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLl

Rais wa Ujerumani, Horst Köhler, yumo nchini Paraguay, kituo chake cha kwanza katika ziara yake ya siku 12 katika nchi za Amerika Kusini.

Akizungumza baada ya kukutana na mwenyeji wake, Nicanor Duarte Frutos, rais Köhler amesema utandawazi unatakiwa kuwaruhusu watu wote duniani kunufaika kutokana na maendeleo ya kiuchumi.

Aidha rais Köhler amesema umaskini ni sababu kubwa ya pekee ya ugaidi na uhalifu na akawatolea mwito viongozi wa kisiasa na wa kibiashara washirikiane kutafuta usawa wa kijamii.