1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Annan kusuluhisha mzozo wa uchaguzi Kenya

10 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cnpq

NAIROBI

Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan atasuluhisha mzozo wa urais wa Kenya uliopelekea umwagaji mkubwa wa damu.

Umoja wa Afrika umesema katika taarifa leo hii kwamba Rais Mwai Kibaki na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wamekubaliana kutafuta uvumbuzi wa amani kwa mzozo huo. Taarifa hiyo imetolewa wakati Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Ghana John Kufour akiondoka nchini humo baada ya kushindwa kuwakutanisha Rais Kibaki na Odinga.

Takriban watu 600 wameuwawa na wengine 260,000 wamepotezewa makaazi yao katika ghasia zilizozuka nchini kote ambazo kwa haraka ziligeuka kuwa visasi vya kikabila kufuatia uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.