ANKARA:Koksal Toptan apendekezwa kugombea wadhifa wa spika na AKP | Habari za Ulimwengu | DW | 09.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ANKARA:Koksal Toptan apendekezwa kugombea wadhifa wa spika na AKP

Chama tawala nchini Uturuki cha AK hapo jana jioni kimewasilisha jina la Koksal Toptan kuwa mgombea wa chama chake katika wadhifa wa spika wa bunge.

Chama hicho kimempendekeza bwana Toptan kwakuka ni mtu mwenye msimamo kadirifu.Uchaguzi wa bunge wa kumchagua spika utafanyika leo hii .Toptana atapambana na wagombea wengine wawili Tunca Toskay ambaye amependekezwa na chama cha mrengo wakulia cha NAP na Kamer Genc mgombea binafsi ambaye aliwahi kuwa naibu spika wa bunge katika miaka ya tisini.Baada ya uchaguzi huu wa spika wa bunge na manaibu wake bunge sasa litakaa chini kumchagua rais mpya wa taifa.Uturuki ilitumbukia kwenye mzozo wa kisiasa baada ya chama cha AK kushindwa miezi Aprili na Mei kulishawishi bunge katika kumpitisha waziri wake wa mambo ya nje Abdulla Gul kuwa rais wa nchi hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com