ANKARA : Papa aendelea na ziara Uturuki | Habari za Ulimwengu | DW | 29.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ANKARA : Papa aendelea na ziara Uturuki

Morgan Tsvangirai anasemekana amejeruhiwa vibaya sana kichwani

Morgan Tsvangirai anasemekana amejeruhiwa vibaya sana kichwani

Papa Benedikt wa 16 leo yuko katika siku ya pili ya ziara yake nyeti nchini Uturuki ambapo ataelekea kwenye mji wa pwani wa Ephesus na baadae Instanbul.

Akiwa kwenye mji wa Ephesus ambao inaaminiwa kuwa mama wa Yesu Kristo alikwenda kuishi huko siku zake za mwisho Papa huyo wa Kanisa Katoliki ataendesha misa.

Akiwa mjini Instanbul Papa atakutana na Askofu Mkuu Bartholomeo wa Wakristo milioni 250 wa madhehebu ya Orthodox duniani.Mkutano wao huo utakuwa ni sehemu ya juhudi za kuondowa mfarakano kati ya makanisa hayo mawili ulioanzia mwaka 1054.

Wakati huo vita vya msalaba vliteketeza Constantinople ambao hivi sasa ndio mji wa Instanbul.

Hapo jana Papa alikutana na Ali Bardokoglu ambaye ni afisa wa pili mwandamizi wa kidini nchini Uturuki nchi ambayo haina mafungamanio rasmi na dini yoyote ambaye alishutumu vikali matamshi yaliyotowalewa na Papa kuhusu Uislamu hapo mwezi wa Septemba.

Katika mazungumzo yake ya hapo jana Papa Benedikt ametowa wito wa kuwepo kwa majadiliano ya dhati kati ya Wakristo na Waislamu.

Maelfu ya Waturuki waliandamana kupinga ziara ya Papa Benedikt kutokana na kukariri matamshi ya mfalme wa kale aliyehusisha Uislamu na matumizi ya nguvu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com