1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMMAN: Bush na al-Maliki watafuta suluhu la machafuko ya Irak

30 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnx

Rais George W.Bush wa Marekani amemsifu waziri mkuu wa Irak Nuri al-Maliki,baada ya viongozi hao kukutana katika mji mkuu wa Jordan,Amman.Kabla ya mkutano huo,sauti zilipazwa nchini Marekani kuilamu serikali ya Irak kuwa inashindwa kuzuia machafuko yanayozidi nchini humo.Waziri mkuu al-Maliki amehakikisha kuwa ataimarisha juhudi zake za kutaka kuleta upatanisho wa taifa.Wakati huo huo Bush alisisitiza kuwa mapambano kati ya Washia na Wasunni yatazidi ikiwa Irak itagawika.