AMMAN: Bush na al-Maliki wamekutana nchini Jordan | Habari za Ulimwengu | DW | 30.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

AMMAN: Bush na al-Maliki wamekutana nchini Jordan

Rais George W.Bush wa Marekani amekutana na waziri mkuu wa Irak,Noori al-Maliki kwa azma ya kutafuta njia ya kukomesha machafuko yanyozidi nchini Irak.Baada ya kuwa na mkutano huo katika mji mkuu Amman nchini Jordan,Bush alisema Marekani itabakisha vikosi vyake Irak ilimradi serikali ya Baghdad inaomba hivyo.Kwa upande mwingine waziri mkuu al-Maliki amevunjika moyo kuwa vikosi vya usalama nchini Irak bado havijaweza kukomesha mashambulio ya wanamgambo nchini humo.Saa chache kabla ya mkutano huo,kundi la wabunge linaloongozwa na Moqtada al-Sadr mwenye mrengo mkali,walikataa kushiriki katika serikali ya Irak wakiupinga mkutano kati ya Bush na al-Maliki.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com