Amman. Abbas anasema matumaini bado yako kwa mazungumzo ya serikali ya umoja.
15 Oktoba 2006Matangazo
Rais Mahmoud Abbas ameeleza masikitiko yake leo kwa kuendelea hali ya mgawanyiko baina ya chama chake cha Fatah na Hamas , akisema kuwa bado kuna nafasi ya mazungumzo ya kuunda umoja.
Chama cha Hamas kinaongoza serikali ya nchi hiyo baada ya ushindi wa kishindo wa bunge mwezi wa januari.
Msaada wa kimataifa wa fedha katika mamlaka hiyo ya Wapalestina umesitishwa kutokana na chama cha Hamas kushindwa kutangaza kujiweka mbali na matumizi ya nguvu pamoja na kuitambua Israel kuwepo.