1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ALGIERS : Wasalafist wadai kuhusika na shambulio la bomu

12 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCkA

Kundi la wanamgambo wa Kiislamu linalojiita „Kundi la Salafist la Kuhubiri na Kupambana“ limedai kuwa ndio lililohusika na shambulio la bomu,kama kilomita 10 magharibi ya mji mkuu Algiers.Shambulio hilo lilifanywa siku ya Jumapili dhidi ya basi lililokuwa likisafirisha wafanyakazi wa kigeni wa kampuni la mafuta.Dreva wa basi aliuawa na wafanyakazi tisa walijeruhiwa. Wakuu wa makampuni ya mafuta wamesema, wataimarisha usalama lakini hawakueleza zaidi.