ABU DHABI:Kansela Merkel aunga mkono juhudi za upatanishi za Saudi Arabia | Habari za Ulimwengu | DW | 06.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ABU DHABI:Kansela Merkel aunga mkono juhudi za upatanishi za Saudi Arabia

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesisitiza dhima ya Umoja wa Ulaya katika utaratibu wa kutafuta suluhisho la amani kati ya Israel na Wapalestina.Akizungumza katika mji mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu,Abu Dhabi,Merkel amesema kuna haja ya kuwa na mtazamo wa kishujaa wenye suluhisho la kuwa na mataifa mawili.Israel inapaswa kuwa na hakika ya usalama,mipakani mwake na Wapalestina nao wanahitaji kupewa matumaini ya kiuchumi.Akaongezea kuwa anaunga mkono jitahada za Saudi Arabia kutafuta suluhisho la mgogoro wa makundi mawili hasimu ya Kipalestina,Hamas na Fatah.Merkel akiendelea na ziara yake ya Mashariki ya Kati,leo hii anazitembelea Dubai na Kuwait.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com