1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABIDJAN: Kiongozi wa zamani wa waasi ni waziri mkuu mpya

5 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCY

Kiongozi wa zamani wa kundi la waasi nchini Ivory Coast ameapishwa kuchukua wadhfa wa waziri mkuu.

Guillaume Soro aliyelidhibiti eneo la kaskazini mwa Ivory Coast kwa miaka minne amesema kuwa lengo lake kuu ni kutafuta amani ya kudumu.

Amepewa wadhfa huo wa waziri mkuu kufuatia makubaliano ya amani ya Burkinafaso ya mwezi uliopita.

Jaribio la kumpindua rais Laurent Gbagbo lililoshindwa miaka mitano iliyopita ndio chanzo cha machafuko nchini Ivory Coast.

Wanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa mataifa na kikosi cha Ufaransa bado wanapiga doria katika eneo la amani baina ya pande hizo mbili.