1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Özil akamilisha uhamisho Fenerbahce

25 Januari 2021

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani Mesut Özil amekamilisha uhamisho wake kutoka Arsenal na sasa amejiunga na miamba wa Uturuki Fenerbahce.

https://p.dw.com/p/3oNv5
Fußball Deutschland Türkei Mesut Özil wechselt zu Fenerbahce Istanbul
Picha: AP/dpa/picture alliance

Klabu hiyo imesema Özil amekubali kutia saini mkataba wa miaka mitatu na nusu baada ya kujiunga nao bila ada yoyote.

Özil aliyewahi kuichezea Real Madrid pia alikuwa ameachwa kabisa nje ya kikosi cha Arsenal kwa mashindano yote msimu huu ila aliendelea kuishabikia klabu hiyo katika mitandao ya kijamii.