Zoezi la Uandikishaji wapiga kura visiwani Zanzibar
14 Septemba 2009Matangazo
Zoezi la kuandikisha wapiga kura kwenye daftari la kudumu la wapiga kura linaendelea visiwani Zanzibar kukiwa bado na matatizo yanayojitokeza na hali ikielezwa kuwa mbaya katika kisiwa cha Pemba. Kutokana na hali hiyo Majeshi ya usalama yameimarishwa kisiwani humo. Grace Kabogo amezungumza na mwandishi wetu Salma Said akiwa Pemba na alianza kwa kumuuliza hali halisi ikoje kisiwani humo.