Zoezi la kupiga kura Sudan laingia siku ya pili hii leo
12 Aprili 2010Matangazo
Uchaguzi nchini Sudan umefanyika kwa siku ya pili hii leo, huku tume ya uchaguzi ikitangaza kurefusha zoezi la kupiga kura kwa siku mbili ili kuzuia kuwafungia raia kupiga kura kutokana na matatizo ya kiufundi. Josephat Charo alizungumza na bwana Ibrahim Himid, mkaazi wa mjini Khartoum, na kwanza kumuuliza hali ilivyo mjini humo.
Mtayarishaji: Josephat Charo
Mhariri: Othman Miraji