1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zimbabwe yatangaza ukame nchini humo kuwa janga la taifa

3 Aprili 2024

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangaza ukame nchini humo kuwa janga la kitaifa. Mnangagwa ameongeza kwamba nchi hiyo inahitaji zaidi ya dola bilioni mbili kuwalisha mamilioni ya watu wanaokabiliwa na njaa.

https://p.dw.com/p/4eOna
Zimbabwe
Ukame ZimbabwePicha: Privilege Musvanhiri/DW

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa leo ametangaza ukame nchini humo kuwa janga la kitaifa. Katika taarifa, Mnangagwa ameongeza kwamba nchi hiyo inahitaji zaidi ya dola bilioni mbili kuwalisha mamilioni ya watu wanaokabiliwa na njaa. 

Taarifa ya Mnangagwa inafuatia matangazo kama hayo yaliyotolewa na Zambia na mwishoni mwa mwezi Februari na Malawi mnamo mwezi Machi, wakati ukame uliosababishwa na hali ya El Nino inayoikumba dunia, ukileta mzozo wa kibinadamu kusini mwa Afrika. Wakulima wakabiliwa na ukame Kusini mwa Jangwa la Sahara

Rais huyo wa Zimbabwe ameongeza kwamba, zaidi ya watu milioni 2.7 nchini Zimbabwe watakumbwa na njaa mwaka huu, kwa kuwa asilimia 80 ya nchi hiyo haikupata mvua za kutosha.