1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina barani Ulaya

Oummilkheir23 Februari 2007

Kansela Angela Merkel awasihi wapalastina waonyeshe ishara ya kujongeleana na kuaminiana pamoja na Israel kwa kumuachia huru Schalid

https://p.dw.com/p/CHJN
Kitambulisho cha amani ya Mashariki ya kati
Kitambulisho cha amani ya Mashariki ya kati

Kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina,Mahmoud Abbas amekua na mazungumzo hii leo pamoja na kamnsela Angela Merkel mjini Berlin.Kabla ya hapo Mahmoud Abbas alizungumza na waziri wa mambo ya nchi za nje Frank-Walter Steinemeir.

Kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina aliyewasili jana mjini Berlin, anasaka uungaji mkono wan chi za magharibi kwa makubaliano ya Makka ambapo Fatah na hamas wamekubaliana kushirikiana kuunda serikali.Muhimu zaidi katika ziara hii ya rais Mahmoud Abbas nchini Ujerumani ni kujaribu kuusihi Umoja wa Ulaya ukubali kuisaidia kifedha serikali ya Palastina.

Wakizungumza na waandishi habari mwishoni mwa mazungumzo yao mjini Berlin,kansela Angela Merkel ametilia mkazo masharti ya jumuia ya kimataifa kwa Hamas akiwahimiza wakati huo huo wapalastina wamuachie huru haraka mwanajeshi wa kiisrael Gilad Schalid,ili kuonyesha ishara njema ya kujongeleana na kuleta hali ya kuaminiana.

Rais Mahmoud Abbas amezungumzia umuhimu wa kubadilishana wafungwa kati ya Israel na Palastina.

Jana usiku kiongozi huyo wa utawala wa ndani wa Palastina alikua na mazungumzo pamoja na waziri wa mambo ya nchi za nje wa serikali kuu ya Ujerumani Frank-Walter Steinemeier.

Mwishoni mwa mazungumzo hayo,Mahmoud Abbas alionekana kua na matumaini mema,kwamba huenda pengine umoja wa ulaya ukaondowa hivi karibuni vizuiwizi vya fedha dhidi ya serikali ya Palastina.

“Tuko karibu sana” amesema Mahmoud Abbas akimaanisha hawako mbali kufikia makubaliano.

Kabla ya hapo kiongozi huyo wa utawala wa ndani wa Palastina alisema,tunanukuu:

“Tunahakikisha,tunaunga mkono fikra ya kuwepo madola mawili jirani-fikra ya kuwepo dola huru la Palastina litakalokua jirani na dola la Israel.Na tunawajibika na kuahidi kuachana na matumizi ya nguvu na visa vya kigaidi.”

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinemeier amemuahidi rais Mahmoud Abbas watasaidia kutia njiani makubaliano ya Makka.Baada ya mazungumzo yao waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier amesema tunanukuu:

“Ni matumaini yetu kuona kwamba makubaliano yaliyofikiwa yanaweka msingi madhubuti wa kukoma matumizi ya nguvu kat

ika Palastina.”Mwisho wa kumnukuu.

Kiongozi wa Utawala wa ndani wa Palastina ataondoka Berlin hivi punde na kuelekea Brussels kwa mazungumzo pamoja na mkuu wa siasa ya nje ya Umoja wa Ulaya Javier Solana,kabla ya kwenda Paris ambako kesho ataonana na rais Jacgue Chirac wa Ufaransa.