Zelaya ajipenyeza kwa siri kurudi Honduras .
22 Septemba 2009TEGUCIGALPA.
Rais aliepinduliwa nchini Honduras Manuel Zelaya amerejea nchini humo kisirisiri na ameomba hifadhi kwenye ubalozi wa Brazil katika mji mkuu wa nchi hiyo Tegucigalpa.
Zelaya alierejea nchini jana anapigania kurudi katika mamlaka kwa njia ya maandamano na mgomo wa nchini kote.
Bwana Zelaya mwenyewe amehakikisha kwamba hapatakuwa na matumizi ya nguvu na ametoa mwito wa kufanyika mdahalo baina ya matabaka yote ya jamii nchini Honduras.
Wakati huo huo kiongozi wa kipindi cha mpito nchini Honduras ameutaka ubalozi wa Brazil umtoe bwana Zeleya na umkabidhi kwa serikali.
Na habari kutoka New York zinasema waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton ametoa mwito juu ya kufanyika mazungumzo ili kuepusha umwagikaji damu nchini Honduras wakati serikali ya mpito imetangataza amri ya kutotoka nje na pia imefunga uwanja wa ndege.