Zanzibar:Hali ya uandikishaji kwenye daftari la kudumu kisiwani Tumbatu
22 Septemba 2009Matangazo
Jana ilibidi polisi watumie mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya watu wanaosemekana walikivamia kituo cha uandilishaji wapiga kura. Maafisa wa chama cha upinzani cha CUF Visiwani Zanzibar wanasema wengi wa wafuasi wao wamekataliwa kupewa haki ya kujiandikisha kuwa wapiga kura.
Othman Miraji amezungumza kwa njia ya simu na mkaazi wa Kisiwa cha Tumbatu, Shamata Akida, kutaka kujua hali ilivyo...
Mtayarishaji: Othman Miraji
Mhariri: Mohamed Abdulrahman