1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Zanzibar: Mwandishi wa Habari anatakiwa kuwa na Kibali cha kufanya kazi

Idara ya habari maelezo Zanzibar imesema kuanzia tarehe mosi mwezi ujao ni lazima kila mwandishi wa habari visiwani humo awe na kibali cha kuonesha yeye ni mwandishi kabla ya kuandika au kufanya kazi yake kama mwandishi.

Kibali chatakiwa Zanzibar kabla ya Mwandishi kufanya shughuli za Uandishi

Kibali chatakiwa Zanzibar kabla ya Mwandishi kufanya shughuli za Uandishi

Lakini tayari waandishi visiwani humo wameanza kulalamika wakisema kuwa hii ni njia moja ya kuwakandamiza waandishi habari kwa kuwa kuna wengine ambao wameomba kupata vibali hivyo na hadi sasa hawajavipokea.

Amina Abubakar amezungumza na mkurugenzi wa idara ya habari visiwani humo aliyetoa taarifa hiyo Omar Chunda na kwanza anaeleza zaidi kuhusu sheria hii.

(Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri: Yusuf Saumu

Sauti na Vidio Kuhusu Mada