Zanzibar: Mivutano iliyopo katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
22 Oktoba 2009Matangazo
Mwanzoni mwa wiki hii Kamati ya Uchunguzi ya chama tawala cha CCM nchini Tanzania ilikuwa visiwani Zanzibar kutafuta maoni ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kufuatia mivutano iliyopo baina ya wajumbe hao na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Grace Kabogo amezungumza na Hamza Hassan Juma, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Kiongozi wa Zanzibar, na alianza kuelezea kile kilichojitokeza katika mazungumzo baina ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Kamati hiyo inayojulikana kama kamati ya Mwinyi.
Mtayarishaji: Grace Patricia Kabogo
Mhariri: Mohamed Abdulrahman