Zanzibar: Kujiuzulu kwa waziri wa Miundo Mbinu na Mawasiliano | Matukio ya Afrika | DW | 24.07.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Zanzibar: Kujiuzulu kwa waziri wa Miundo Mbinu na Mawasiliano

Waziri wa Miundo Mbinu na Mawasiliano wa Zanzibar Hamad Masoud Hamad amesisitiza kwamba hatua yake ya kujiuzulu kutoka wadhifa huo haitokani na shinikizo lolote jinsi inavyodhaniwa na wengi.

Kujiuzulu kwa Waziri wa Miundo Mbinu na Mawasiliano kunatokana na ajali ya meli

Kujiuzulu kwa Waziri wa Miundo Mbinu na Mawasiliano kunatokana na ajali ya meli

Anasema alifanya uamuzi huo baada ya mazungumzo na viongozi husika. Nafasi yake imechukuliwa na Rashid Seif Suleiman ambaye ni mwakilishi wa wa jimbo la Ziwani kutoka chama cha CUF. Bw Hamad aliliarifu Baraza la Wawakilishi juu ya uamuzi wake wa kujiuzulu .

Jee wananchi huko Zanzibar wameipokeaje hatua ya kujiuzulu kwa waziri huyo hamad Masou Hamad ? Mwandishi wetu Salma Said ametukusanyia maoni ya baadhi yao.

(Kusikiliza maoni hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: Salma Said

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada