1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zabuni ya uchapishaji wa karatasi za kura yazua utata Kenya

Daniel Gakuba22 Juni 2017

Mvutano umeshamiri kati ya kambi kuu mbili za kisiasa Kenya, kuhusu zabuni ya uchapishaji wa karatasi za upigaji kura, iliyopewa kampuni ya al-Ghurair ya huko Dubai. Muungano wa upinzani wa NASA umetishia kususia uchaguzi ikiwa zabuni hiyo haitatenguliwa, lakini IEBC imesema haitetereshwi na kitisho hicho. Sikiliza majadiliano na George Musamali, mchambuzi wa siasa aliyeko mjini Nairobi.

https://p.dw.com/p/2f3AV