1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

YOUNDE:Chama tawala chashinda uchaguzi nchini Cameroon

Chama cha Rais Paul Biya cha Democratic Rally of the Cameroonian People RDPC kimepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa bunge na serikali za mitaa nchini Cameroon uliyofanyika Jumapili iliyopita.

Chama hicho kimepata viti 152 kati ya viti 180 bungeni, ambapo katika bunge linalomaliza muda wake kilikuwa na viti 149.

Chama kikuu cha Upinzani cha SDF kinachoongozwa na John Fru Ndi kimepata viti 14.

Hata hivyo upinzani umelalamika kuwa kulikuwa na ghilba na umetangaza kuyapinga matokeo hayo mahakamani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com