1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YAOUNDE:Rais Jintao wa Uchina azuru Cameroun

31 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCWR

Rais wa Uchina Hu Jintao anaanza ziara rasmi ya mataifa nane barani Afrika.Hii ni ziara ya tatu ya kiongozi huyo barani Afrika tangu mwaka 2003 aliposhika wadhifa huo.Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kisiasa.Rais Jinato anakutana na Rais wa Cameroon Paul Biya hii leo vilevile kutia saini makubaliano ya ushirikiano .

Kiongozi huyo anapanga kuzuru nchi ya Sudan anakotarajiwa kushinikiza serikali ya Khartoum kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika juhudi za kumaliza ghasia katika eneo la magharibi la Darfur.

Kwa mujibu wa Marekani eneo hilo lililo na utajiri wa mafuta mengi linakabiliwa na ghasia zinazoelezwa kuwa mauaji ya halaiki.Nchi ya Sudan ni ya tatu anayotarajiwa kuzuru Bwana Jintao.

Nchi yaUchina inadhaniwa kuwa ina uwezo wa kuishawishi serikali ya Sudan kukubali hatua ya kupeleka majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa kwasababu ya uhusiano wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili.

Ziara hiyo inaonyesha namna nchi ya Uchina inataka kujishughulisha na shughuli za ushirikiano wa kiuchumi baraani Afrika.Kiongozi huyo aidha anatarajiwa kuzuru mataifa ya Liberia,Zambia,Namibia,Afrika Kusini,Msumbiji vilevile Ushelisheli.