1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

YAOUNDE:Chama tawala chapata ushindi mkubwa

Chama tawala nchini Cameroon cha Democratic Rally of the Cameroonian People RDPC kimepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa wabunge na mabaraza ya miji kwa mujibu wa matokeo ya kwanza ya jana usiku.Chama hicho cha RDPC kinaongozwa na Rais Paul Biya na kilipata nafasi 152 ya viti vyote bungeni vilivyo 180.

Vyama vya upinzani vinaonya kuwa endapo chama hicho kinapata thuluthi mbili ya kura zote bungeni huenda katiba ikafanyiwa marekebisho ili kumruhusu Rais Biya kugombea tena urais ifikapo mwaka 2011.Kiongozi huyo amekuwa madarakani tangu mwaka 82.

Chama cha Social Democratic kina nafasi 14 huku Cameroonian Democratic Union kina nafasi 4.Chama cha Progressive Movement kimejinyakulia nafasi moja bungeni.

Chama cha National Union for Democracy and Progress kinachounga mkono serikali kimepata nafasi 2.Nafasi saba bado hazijapata wawakilishi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com