1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YANGON:Wanajeshi wapelekwa katikati ya mji kwa hofu ya kuzuka maandamano mapya

26 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7CY

Serikali ya kijeshi ya Myanmar imewapeleka wanajeshi wake katikati ya mji wa Yangon kuyazingira maeneo matakatifu ya Kibuddha kwa kuhofia huenda maandamano mapya yakazuka.

Leo ni ijumaa ya mwisho ya masikitiko kwa madhehebu ya Buddha na ni mwezi mmoja kamili tangu watawa wa Kibuddha walipoingia mabarabarani kuanzisha maandamano ya kuunga mkono demokrasia dhidi ya utawala wa kijeshi.

Wakati huo huo televisheni ya taifa imethibitisha kuwa kiongozi wa upinzani Aung San Su Kyi anayetumikia kifungo cha nyumbani amekutana na muwakilishi wa serikali ya kijeshi ya Myanmar hata hivyo walichokijadili bado hakijulikani.