1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

YANGON:Mwakilishi wa UN hataongezwa mkataba wake

Uongozi wa kijeshi nchini Myanmar umeamua kutoongeza muda wa afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa kufuatia kauli ya shirika hilo kuhusu umasikini.Kwa mujibu wa afisa wa mawasiliano wa Umoja wa mataifa Aye Win; mwakilishi wa Shirika hilo nchini humo Charles Petrie alipokea taarifa hizo baada ya kufika katika mji mkuu mpya wa Naypyidaw.

Uamuzi huo wa serikali huenda ukamlazimu afisa huyo wa Umoja wa mataifa kuondoka nchini humo.Mkataba wake ulianza mwaka 2003.Serikali ya kijeshi ya Myanmar imeghadhabishwa na kauli ya mwezi jana ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali mbaya ya maisha nchini humo.

Bwana Petrie aidha alitoa kauli Fulani zilizoshtumu viongozi wa serikali ya Myanmar baada ya waandamanaji kushambuliwa na serikali.Hatua hiyo ya dharura inatokea siku moja kabla ya mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Ibrahim Gambari kuwasili nchini humo kwa mazungumzo na viongozi wa serikali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com