1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YANGON:Gambari awasili Myanmar kujaribu kutanzua mzozo wa kisiasa

30 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLV

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ibrahim Gambari amewasili nchini Myanmar kwa mazungumzo na wakuu wa kijeshi wa nchi hiyo kujaribu kumaliza mzozo wa kisiasa uliyoikumba nchi hiyo.

Utawala huo wa kijeshi ulilazimika kutumia nguvu kusambaratisha maandamano ya wananchi wakiongozwa na watawa wa Kibuddha wanaodai kuwepo kwa demokrasia nchini humo.

Katika hatua hiyo kiasi cha waandamanaji 13 waliuawa huku mamia kadhaa wakikamatwa.

Hata hivyo pamoja na kutokuwepo kwa idadi kubwa ya watu mitaani lakini, baadhi ya mitaa ya mji mkuu Yangon imeshuhudia baadhi ya watu wachache wakiendelea na maandamano hayo ya amani.

Serikali ya Singapore moja ya nchi za Umoja wa Kusini Mashariki mwa Asia, ASEAN ambao Myanmar ni mwanachama imelezea matumaini yake juu ya ziara hiyo ya Ibrahim Gambari.