Wingu la jivu la volkanu laendelea kuchafua misafara ya ndege
18 Aprili 2010Lakini, safari za ndege za majaribio zilizofanywa nchini Uholanzi na Ujerumani, ikidhihirika bila dhara zozote, zatoa matumaini mema.
Nchi nyingi zimepiga marufuku misafara ya ndege katika anga zao hadi usiku wa manane leo Jumapili au kesho Jumatatu . Hii imewafanya maalfu ya abiria kunasa sehemu mbali mbali ulimwenguni.
Mtaalamu wa utabiri wa hali ya hewa, Helmut Malewski amearifu kwamba wingu hilo la jivu yamkini lisienee mbali zaidi.
Uingereza, imepanua marufuku ya misafara yake mingi ya ndege, hadi saa mbili leo usiku. Anga ya Ujerumani, kwa misafara ya ndege, itafungwa kwa misafara hadi alao alasiri ya leo.
Magari moshi zaidi yanatumika sehemu mbali mbali za Ujerumani, ili kukidhi mahitaji ya wasafiri wasioweza kusafiri kwa ndege. Maafisa wa mashirika ya ndege wanarifu kwamba, hasara waliopata inapindukia Euro milioni 150 kwa siku.
Mwandishi: Ali,Ramadhan
Mhariri: P.Martin