1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WINDHOEK:Mataifa ya magharibi yakashifu uongozi wa Zimbabwe

Mataifa ya magharibi yanasisitiza kuunga mkono vyama vya upinzani nchini Zimbabwe huku Rais Mugabe akitisha kuwafurusha mabalozi wa mataifa ya kigeni wanaoendelea kumkashifu.Waziri wa maendeleo wa Ujerumani Heidemarie Wieczorek-Zeul anatoa wito kwa nchi jirani kushtumu uongozi wa Rais Mugabe unaokiuka haki za binadamu.

Wakati huohuo Rais wa Zambia Levy Mwanawasa anatoa wito kwa mataifa wanachamama wa Jumuiya ya Maendeleo ya mataifa ya Afrika Kusini, SADC kuingilia kati suala hilo na kujadilia matatizo yanayokumba Zimbabwe.

Hata hivyo kiongozi huyo aliyekuwa ziarani kwa siku tano nchini Namibia anaongeza kuwa mataifa yasiyo wanachama wa jumuiya hiyo ya SADC yasihusike.

Zimbabwe inalaumu mataifa ya magharibi kwa kuingilia nchi yake kufuatia shutma kutoka Umoja wa Ulaya,Uingereza na Marekani baada ya kushambulia wanasiasa wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change ,MDC.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com