William Ruto afutiwa mashitaka ya ufisadi | Matukio ya Afrika | DW | 13.04.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

William Ruto afutiwa mashitaka ya ufisadi

Mahakama Kuu nchini Kenya imefuta mashtaka ya ufisadi yaliyokuwa yakimkabili waziri wa zamani wa elimu ya juu, William Ruto, baada ya kukosekana kwa ushahidi. Ruto ni miongoni mwa wanasiasa wanaoshitakiwa pia na ICC.

Yaliyotokea Kenya 2007

Yaliyotokea Kenya 2007

Ruto na watu wengine wawili walikuwa wakituhumiwa kuliibia Shirika la Usafishaji Mafuta la Kenya zaidi ya dola milioni 1 kwa kuliuzia ardhi ya eneo la hifadhi ya misitu.

Uamuzi wa kumvua Ruto kwenye mashitaka hayo, unakuja siku moja tu baada ya mwanasiasa huyo kurejea nyumbani kutoka kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu yenye makao yake makuu mjini The Hague, Uholanzi, ambako anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu, kutokana na vurugu za baada ya uchaguzi hapo mwaka 2007.

Swala kubwa ambalo hivi sasa watu wengi nchini Kenya wanajiuliza, ni iwapo Ruto atarejeshwa katika nafasi yake ya uwaziri. Aboubakar Lyongo amezungumza na mwanasheria wa kujitegema, Harun Ndubi, kutaka ufafanuzi zaidi wa kisheria katika suala hilo.

Mahojiano: Aboubakary Liongo/Harun Ndubi
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman

DW inapendekeza