1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

120211 Westerwelle Sicherheitsrat

Sekione Kitojo12 Februari 2011

Waziri wa mambo ya kigeni ya Ujerumani Guido Westerwelle ameyataka mataifa ya Kiarabu kuingia zaidi katika utaratibu zaidi wa kidemokrasia, baada ya kuangushwa utawala wa Mubarak

https://p.dw.com/p/10GDM
Rais aliyeondolewa madarakani nchini Misri Hosni MubarakPicha: picture-alliance/dpa

Ujerumani inakalia kwa mara ya kwanza kiti katika baraza la usalama la umoja wa mataifa. lakini matukio nchini Misri ambapo rais Hosni Mubarak amejiuzulu kutoka madarakani, yamefunika hatua hiyo ya Ujerumani kujiunga na baraza hilo la usalama la umoja wa mataifa. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle akiwa mjini New York kuzindua kuingia kwa Ujerumani katika baraza hilo, amekaribisha uamuzi wa rais Mubarak , baada ya wiki kadha za maandamano na kuyataka mataifa ya Kiarabu kuingia zaidi katika utaratibu wa kidemokrasia. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon ametoa wito wa kuwapo utaratibu wa amani katika hatua za mpito kuelekea demokrasia zaidi.

Si kwa kutumia hali ya utaratibu mzuri wa baraza la usalama la umoja wa mataifa , kuhusiana na majadiliano ya mada zilizopo. Ambapo wanachama 15 wa baraza hilo la umoja wa mataifa wakijadili suala la amani ya kimataifa pamoja na usalama, kunakuwa na hali ndogo ama kubwa ya mivutano katika majadiliano yao ambayo yamekwisha tayarishwa mapema , hali ambayo haikuwapo katika mitaa ya mjini Cairo , ambapo waandamanaji waliweza kuzika enzi ya utawala. Ni kwa njia ambazo si rasmi, ni kwa ujumbe mfupi wa simu za mkononi, barua pepe katika mtandao wa internet, ambazo zimeweza kukamilisha hatua ya kumlazimisha Hosni Mubarak kujiuzulu. Taarifa hizo zimemlazimisha waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle , kusitisha kwa muda kujitokeza kwake katika baraza la usalama kwa mara ya kwanza na kusema.

Münchner Sicherheitskonferenz - Westerwelle
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido WesterwellePicha: Picture-Alliance/dpa

Tumefurahi, kwamba sasa njia iko wazi kwa mwanzo mpya wa kisiasa, kuelekea katika demokrasia na kuleta amani ndani na nje ya nchi hiyo.

Ni baina ya furaha na shauku , ambapo maneno ya waziri wa mambo ya kigeni yalikuwa yanaonesha, na usiku baada ya hotuba iliyokatisha tamaa ya Mubarak Alhamis usiku, Westerwelle alieleza wasi wasi wake kuhusu utatuzi wa amani katika mzozo huo wa Misri. Baada ya hapo ambapo ilikuwa ni hatua ya ghafla na ya mshangao, waziri Westerwelle amerejea pendekezo lake, la kuunga mkono ujenzi mpya wa mfumo mpya wa kisiasa.

Utawala wa Ujerumani uko tayari, amesema Westerwelle pembezoni mwa ushirika wao wa karibu kusaidia mabadiliko hayo ya kidemokrasia. Lakini pia shauku kuhusiana na kuondoka madarakani kwa Mubarak inaweza kuporomoka kutokana na hali jumla ambayo haieleweki kuhusiana na suala la , nani na kitugani kinakuja baada ya hapa.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito, kama anavyosema , wa utaratibu wa uwazi na ulioratibiwa kwa njia sahihi katika kipindi hiki cha mpito, kutekeleza matarajio halali ya umma wa Misri.

UN Generalsekretär Ban Ki Moon bei einer Pressekonferenz mit Bundespräsident Christian Wulff in Berlin zu den Ereignissen in Ägypten Kairo Mubarak
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moonPicha: AP

Ni muhimu , kwamba haki za binadamu na uhuru wa raia vinaheshimiwe bila kuwekewa mipaka.

Amesema Ban na kuongeza.

Naupongeza uamuzi mgumu aliochukua Mubarak kwa maslahi ya umma wa Misri.

Dunia pamoja na wadau wanatoa wito upatanishi wa kweli. Ni hakika kwa Berlin sio tu imeanza ushirikiano wa kweli na Tunisia , lakini pia watakuwa na mahusiano mazuri na Misri na kutafuta washirika muhimu wa mazungumzo katika serikali pamoja na upande wa upinzani.

Mwandishi: Schmidt, Thomas / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri : Mohammed Dahman