Westerwelle ataka msimamo wa EU kuhusu Belarus | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 03.01.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Westerwelle ataka msimamo wa EU kuhusu Belarus

Msimamo huo ni kuhusu ukandamizaji unaoendelea chini ya uongozi wa Rais Alexander Lukashenko wa Belarus.

default

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle amesema kuwa Umoja wa Ulaya unatakiwa kutoa jibu la wazi la kisiasa juu ya ukandamizaji unaofanywa chini ya utawala wa Rais Alexander Lukashenko nchini Belarus. Matamshi hayo ni kwa mujibu wa gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung.

Westerwelle amesema Umoja wa Ulaya unatakiwa kukabiliana na uongozi wa kisiasa wa Belarus kutokana na taarifa za rushwa katika uchaguzi na ukandamizaji nchini humo.

Ujerumani imekuwa miongoni mwa wakosoaji wakali wa Belarus, wakati ambao nchi hiyo inaendelea kuwashikilia mamia ya wafuasi wa upinzani ambao walikamatwa wakati wa maandamano makubwa kupinga uchaguzi wenye utata wa Desemba 19, uliompa ushindi Lukashenko.

Siku ya Ijumaa, Belarus iliamuru kufungwa kwa ofisi ya Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya, kwenye mji mkuu wa Minsk, baada ya shirika hilo kukosoa vikali uchaguzi huo.

 • Tarehe 03.01.2011
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/zsmM
 • Tarehe 03.01.2011
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/zsmM

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com