1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Somalia auwawa

11 Juni 2011

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Somalia, Abdishakur Hassan ameuawa nyumbani kwake katika shambulizi la kujitoa mhanga.

https://p.dw.com/p/11YUn
Wafuasi wa kike wa kundi la waasi la al-ShebabPicha: AP

Ionekanavyo, shambulizi hilo lilifanywa na mpwa wake wa kike. Hiyo ni kwa mujibu wa afisa wa ngazi za juu wa Somalia, Adan Mohamed. Vyanzo vingine vya usalama vinasema mwanamke huyo aliishi katika nyumba ya waziri huyo tangu siku tatu zilizopita.

Kiongozi wa kundi la waasi la al-Shebab ametangaza kuwa wao ndio waliohusika na shambulio lililomuuwa waziri huyo.

Mwandishi: Sudi Mnette

Mhariri: Prema Martin