1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa Iraq ajiuzulu

Admin.WagnerD15 Agosti 2014

Hatimae Waziri Mkuu aliyekuwa aking'ang'ania madarakini nchini Iraq, Nuri al-Maliki jana amejiuzulu wadhfa wake kufuatia shinikizo la ndani ya taifa hilo na nje. Hatua hiyo inafungua njia ya uundwaji wa serikali ya mseto

https://p.dw.com/p/1CvFo
Nuri al-Maliki Rücktritt
Waziri Mkuu wa Iraq aliyejiuzulu Nuri al-MalikiPicha: Reuters

Maliki anafikisha kikomo miaka minane ya mgawanyiko mkubwa, na utawala wa kimadhehebu. Katika taarifa yake ilioneshwa kupitia televisheni kiongozi huyo amemuidhinisha mwenziwe kutoka madhehebu ya Shia Haider al-Abadi aliyekuwa amesimama pembeni yake.

Haya yanatokea wakati ntaifa hilo lilikwa na kitisho kikubwa cha kundi la wanagmbambo wa Kisunni wa Dola la Kiislamu, ambao mpaka sasa wameweza kudhibiti eneo kubwa la kaskazini mwa Iraq. Katika hotuba yake hiyo Maliki alitangaza kufikisha kurahisisha harakati za kisisa na kuundwa serikali mpya na mpinzani wake.

Mapokeo ya Wairaq

Raad Mohammed ni mkazi wa Baghdad "Kukabidhi madaraka kwa waziri mkuu mpya Haider al-Abadi, inatoa ushara ya umuhimu kuwa al Maliki ana nia ya kufanikisha usalama wa Iraq na Wairaq kwa ujumla. Historia itamkumbuka waziri hiyo aliyemaliza muda wake kwa kufanya mengi nchini Iraq".

Irak Bagdad Maliki-Anhänger Demonstration
Raia wa Iraq katika maandamano mjini BaghdadPicha: picture-alliance/dpa

Kwa hakika hotuba ya kiongozi huyo ilikuwa yenye kuonekana kuwatuliza wairaki kutoka jamii ya wachache ya Kisunni, ambao walikuwa wakiitawala Iraq wakati wa utawala wa kibabe wa Saddam Hussein, ambao kwa kiasin kikubwa aliwatenga katika utawala wake jambo ambalo halikutegemewa kabisa pale alipoingia madarakani 2006 kwa nguvu ya Marekani.

Nuri al-Maliki amekuwa akikaidi shinikizo la kumtaka akae chonjo kwa miezi kadhaa kutoka kwa Wassuni, Wakurd, na kiasi fulani cha Washia wenzake na Marekani, amesisitiza haki yake ya kuundwa serikali mpya kwa kuzingatia matokeo ya uchaguzi wa bunge wa mwishoni mwa Aprili.

Misaada ya silaha kwa Wakurd

Katika hatua nyingine duru ambazo hazikutakwa kutajwa jina lake katika vyombo vya habari imesema Uingereza inaonekana yenye uwezekano wa kuzingatia ombi la silaha la wapigajani wa Kikurd kwa lengo la kusaidia kukabiliana na wanamgambo wa Kissuni ambao wanadhibiti sehemu kubwa ya Iraq.

Kwa mujibu wa taarifa za maafisa Marekani iliyaomba matiafa ya Ulaya kutoa msaada wa silaha kwa jeshi la Kikurd. Mataifa kadhaa ikiwemo Ufaransa Ujerumani, Jamhuri ya Czech na Uholanzi zitapeleka silaha kwa Wakurd au kuzingatia uwezekano huo.

Vyanzo hivyo vinasema jeshi hilo la Kikurd halijaomba msaada wa moja kwa moja kwa Uingereza lakini ombi lao linaweza kuzingatiwa bila shka yoyote. Hata hivyo msemaji wa waziri mkuu wa Uingereza hakuweza kupatikana mara moja ili aweze kuzungumzia suala hilo.

Wanajeshi katika eneo lenye nusu mamlaka katika kanda ya Wakurd wanakabiliana vikali na wanamgambo wenye zana kali za kisasa za kivita kutoka kundi lijiitalo Dola ya Kiislamu, ambalo limeweza kudhibiti maeneo ya kaskzani mwa Irq wiki chache zilizopita. Na limekuwa likiwarejesha nyuma wanajeshi hao na kusababisha maelfu ya jamii ya wachache ya Wayazidi, Wakristo kukimbia makazi yao.

Na mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanafanya mkutano wa dharura leo hii mjini Brussels kujadili migogoro mikubwa ukiwemo huo wa Iraq.

Mwandishi: Sudi Mnette RTR

Mhariri: Yusuf Saumu