Waziri Mkuu mpya wa Jordan kutangazwa leo
22 Novemba 2007Matangazo
Waziri mkuu wa Jordan,Marouf al-Bakhit amejiuzulu baada ya kumalizika kwa mamlaka ya baraza lake la mawaziri 26 kufuatia uchaguzi wa bunge.Mfalme Abdallah wa Pili anatazamiwa kumteua waziri wa zamani wa usafiri,Nader al-Dahabi kumrithi al-Bakhit.Waziri Mkuu mpya atatangazwa baadae leo hii,Mflame Abdallah atakaporejea nyumbani kutoka ziara yake ya nchini Misri.