Waumini wafyatuliwa risasi nchini Marekani
10 Desemba 2007Matangazo
Watu 5 wameuawa baada ya kupigwa risasi katika makanisa mawili kwenye jimbo la Colorado nchini Marekani.Katika shambulizi la kwanza watu 4 walipigwa risasi nje ya kanisa kubwa la Kiinjili mjini Colorado Springs.Hapo awali,watu 2 waliuawa na 2 wengine walijeruhiwa,ukingoni mwa mji wa Denver.Katika shambulizi hilo mtu mwenye bunduki aliingia katika kituo cha kuwafunza wamisionari vijana.Polisi hawajui ikiwa kuna uhusiano kati ya mashambulizi hayo mawili.