Watumiaji wa mtandao kutoka Afrika
Ahmed M. kutoka Misri
"Nimeamua kusoma nchini Ujerumani, kwa hiyo nimeanza kutazama kila mara televisheni ya DW."
Bezazel Ferhat kutoka Algeria
"Naitumia DW kwa kuwa ndilo shirika zuri kabisa la kigeni duniani kote. DW hunipa picha kamili kuhusu kila kitu kinachoendelea nchini Ujerumani. Kwangu mimi ni kama dirisha lililo wazi kuelekea Ujerumani, Ulaya na ulimwengu mzima kwa jumla."
Emmanuel kutoka Ghana
"Mbali na vipindi, naipenda DW kwa mahusiano mazuri na wafanyakazi wake, majibu ya haraka ya maswali kutoka kwa wasikilizaji na watumaiji wa mtandao wake pamoja na jinsi inavyotujali."
Ibrahime kutoka Togo
"Matamanio yangu katika siku za usoni ni kuwepo na DW maalumu - kwa ajili ya Afrika pekee."
Mostafa kutoka Marokko
"Uzoefu wangu wa kwanza na DW ni mwaka 1987 wakati nilipokuwa mwanafunzi katika shule ya upili Ujerumani. Nilisikia matangazo ya DW redioni wakati wa usiku, ingawa nilielewa tu kati ya asilimia 2 hadi 5."
Muhammad kutoka Nigeria
"DW kwangu ina maana ya kiunganishi na mataifa mengine kupitia masafa mafupi na mtandao wa intaneti."
Prudence kutoka Benin
"Ningependelea katika siku za suoni DW iwe kama nembo kwa ujuzi wa Ujerumani - kama vile bidhaa nyingi zinazojulikana kama 'Made in Germany'. Kwa miongo kadhaa sasa DW imefaulu kunibadili mimi na wenzangu katika mitazamo yetu mibaya kuhusu Wajerumani ambao wanasemwa mara kwa mara kwa ubaguzi."
Ras Franz kutoka Tansania
"Napenda sana jinsi DW inavyofanya juhudi kubwa kutupasha habari na kutupa taarifa sisi wasikilizaji na wasomaji wa mtandao."
Sadoun kutoka Algeria
"Naitumia DW kwa kuwa vipindi vyake ni tofauti kuliko mashirika mengine ya habari au mitandao. DW inafaulu kutumia ubunifu wake na kwa njia hiyo kuendeleza midahalo na ushirikiano."
Sambadiouma kutoka Guinea
"Kuna vituo vingi vya redio vinavyorusha matangazo barani Afrika. Lakini DW ina umuhimu maalumu kulinganisha na mashirika mengine: Inaturuhusu kutoa maoni yetu."
Samuel kutoka Ghana
"Natumia DW kwa kuwa hunipasha habari za matukio na wafanyakazi wake ni mahiri sana."
Shady kutoka Misri
"Naitumia DW kwa sababu ni shirika bora zaidi ambalo huripoti kila kitu kiukweli na uhakika."