1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu zaidi kuyahama makaazi yao

1 Juni 2012

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi UNHCR limesema katika miaka 10 ijayo, watu wengi duniani watatafuta makaazi nje ya nchi zao au kuwa wakimbizi wa ndani ya nchi zao kutokana na sababu mbali mbali.

https://p.dw.com/p/156L6
Wakimbizi DRCPicha: Reuters

Shirika  la  kuwahudumia  wakimbizi  UNHCR  limesema  kuwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  ukimbizi  wa   kiuchumi, mabadiliko ya tabia nchi , ukosefu wa chakula , na mapigano.

Mkuu wa Shirika hilo la  kuwahudumia  wakimbizi duniani UNHCR Antonio Guterres ametoa sababu nyingine kuwa uhaba wa maji, mashindano ya kutafuta rasili mali na pia ongezeko la watu duniani. Antonio aliyasema hayo alipokuwa akizundua ripoti hiyo katika makao makuu  ya Umoja wa mataifa mjini New York .

Kwa sasa kuna takriban watu milioni 26 waliokosa makaazi ndani ya nchi zao huku idadi ya watu milioni 15-16 wakiwa ni wakimbizi na wengine Millioni moja wakiomba hifadhi  ya  kisiasa katika mataifa ya  nje. Hata hivyo shirika hilo halikutoa idadi ya watu wanaokadiriwa kuongezeka kwa miaka kumi ijayo.

Somali refugees lead their herds of goats home for the night, inside Dagahaley Camp, outside Dadaab, Kenya, Sunday, July 10, 2011. U.N. refugee chief Antonio Guterres said Sunday that drought-ridden Somalia is the "worst humanitarian disaster" in the world after meeting with refugees who endured unspeakable hardship to reach the world's largest refugee camp in Dadaab, Kenya. (Foto:Rebecca Blackwell/AP/dapd)
Maeneo kame nchini KenyaPicha: dapd

Hatua  za  pamoja

Antonio Guterres amesema hili ni suala la kimataifa na linapaswa kutafutiwa suluhisho la kimataifa huku akisisitiza kuwepo pia kwa suluhisho la kisiasa.

"Wakimbizi wengi hungoja suluhu ya kisiasa ipatikane nchini mwao ili waweze kurudi nyumbani na kuishi maisha ya kawaida" lilisema shirika hilo la kuwashughulikia wakimbizi duniani UNHCR.

Wakimbizi  hukabiliwa  na  hali  ngumu ya  maisha

Ripoti hii ya kila mwaka imetoa sura ya  hali halisi ya wakimbizi wa nje ya nchi na wale waliokosa makaazi ndani ya nchi zao. Wakimbizi hujikuta katika hali ngumu ya maisha iliojaa changamoto nyingi hasaa katika suala la kupata suluhisho huku wafanyakazi wa kutoa misaada wanaowasaidia wakikabiliana na vitisho kutoka  maeneo yaliyoathirika.

: Two-year-old, Aden Salaad, looks up toward his mother, unseen, as she bathes him in a tub at a Doctors Without Borders hospital, where Aden is receiving treatment for malnutrition, in Dagahaley Camp, outside Dadaab, Kenya, Monday, July 11, 2011. U.N. refugee chief Antonio Guterres said Sunday that drought-ridden Somalia is the "worst humanitarian disaster" in the world, after meeting with refugees who endured unspeakable hardship to reach the world's largest refugee camp in Dadaab, Kenya. (AP Photo/Rebecca Blackwell)
Ukame na njaa ni sababu za watu kukimbia maeneo yaoPicha: AP

Hata hivyo Mkuu wa UNHCR Antonio Guterres amesema kwa sasa ni nchi nyingi tu zilizofungua mipaka yake kuwapokea wakimbizi ambao nchi zao zinakumbwa na ghasia  na machafuko ikiwemo wale waliokimbia nchi zao kutokana na  maandamano ya kutaka mabadiliko nchini mwao katika maeneo ya kaskazini mwa Afrika na Mashariki ya kati.

Mwandishi :Amina Abubakar/DPA

Mhariri :Mohammed Abdul-Rahman