Watu wawili wamekufa kwa kipindupindu Burundi | Habari za Ulimwengu | DW | 10.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Watu wawili wamekufa kwa kipindupindu Burundi

BUJUMBURA

Watu wawili wamekufa kutokana na kuzuka upya kwa ugonjwa wa kipindupindu kusini mashariki mwa Burundi .

Kwa mujibu wa afisa wa serikali ya mtaa Epimene Batsinda watu wawili wamekufa kutokana na kipindupindu hicho hapo jana na wengine 57 wamelazwa hospitalini katika kituo cha afya cha Ziwa Nyanza kilioko kilomita 130 kutoka Bujumbura .

Amesema takriban watu 151 wameambukizwa ugonjwa huo tokea kuripuka kwake kwa mara ya kwanza hapo Desemba Mosi.

Ameongeza kusema kwamba mripuko wa kipindupindu hutokea mara kwa mara katika mji wa Ziwa Nyanza wenye wakaazi 54,000 kutokana na Ziwa Tangayika kuwa njia pekee ya kujipatia maji ya kunywa na pia kudhibiti afya kwa kuondowa maji taka.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com